Kwa mujibu wa amri hiyo ya rais, katika kipindi cha kwanza, upigaji kura wa uchaguzi huo utafanyika katika mikoa mitano ikiwemo Cairo, Port Said na El-Minya kuanzia tarehe 27 hadi 28 Aprili, katika kipindi cha pili, upigaji kura utafanyika katika mikoa minane ikiwemo Giza, Alexandria na Suez kuanzia tarehe 15 hadi 16, Mei, na katika kipindi cha tatu, upigaji kura huo utafanyika katika mikoa minane ikiwemo Luxor, Qena na South Sinai kuanzia tarehe 2 hadi 3, Juni, na katika kipindi cha mwisho, upigaji kura huo utafanyika katika mikoa sita ikiwemo Assiut na Fayoum kuanzia Juni 19 hadi 20.
Mwezi Juni mwaka jana, mahakama kuu ya Misri ilitoa uamuzi wa kupinga uteuzi wa baraza la chini la bunge la nchi hiyo lililochaguliwa mwanzoni mwa mwaka jana na kutaka livunjwe kwa kuwa baadhi ya vifungu vya sheria ya uchaguzi vinakiuka katiba.